EAST AFRICAN NEWS
ENTERTAINMENT NEWS

WORLD NEWS

TECHNOLOGY
CELEBRITIES NEWS

Share this Post

SPORTS NEWS
HEALTH NEWS

PAMOJA NA UNENE LAKINI HAWEZI ACHA KULA

The Brazilian boy, known only as Misael, was born a healthy 6lb 6oz (2.9kg) But every month since, has gained 6lb (3kg), meaning he str...

29 Sep 2014 | Read more
TOP TEN

Top 10 ‘Breaking Bad’ Moments

Ursula Coyote / AMC 10. The ricin’s fate is revealed For all its discussion over the course of the series, ricin had never been ...

08 May 2014 | Read more
FACTS

WACHINA NOMA SANA

 Ukisikia Wachina balaa sasa hii ni moja wapo, Kiwanda Kimojawapo cha China kijulikanacho kwa jina la LandWind kimeibuka na Kutengene...

25 Nov 2014 | Read more
ENVIRONMENT NEWS

A CLIMATE CHANGE INSPIRED PROJECT LAUNCHES IN DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399 ...

04 Aug 2017 | Read more
FASHION

MH. CATHERINE MAGIGE AZINDUA RASMI DUKA LA ZURII HOUSE OF BEAUTY

. MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige  leo amezindua rasmi  duka ...

12 Jan 2015 | Read more
HISTORY

MAKALA FUPI: Mwanamke aliyehukumiwa kifo Sudan ajifungua

Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuas...

28 May 2014 | Read more
TRAGEDY NEWS

JOCKTAN MAKEKE KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADANI NCHINI NIGERIA

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan...

09 Sep 2017 | Read more

dailyvideo

MKURUGENZI MKUU WA FAO KUZURU TANZANIA, KUFANYA MAQZUNGUMZO NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA SERIKALI, WADAU


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva(pichani), Jumanne wiki hii ataanza ziara rasmi nchini Tanzania ambapo anategemewa kufanya mikutano na mazungumzo na maofisa waandamizi wa serikali na wadau. 

Bw. Graziano da Silva anategemewa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO amepanga kufanya mikutano na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Tanzania Bara), Dkt. Charles Tizeba, na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.

Ziara hii ya Mkurugenzi Mkuu inakuta wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania. Wakati wa ziara hii, Bw. Graziano da Silva atakutana na uongozi na wafanyakazi wa FAO hapa Tanzania kabla ya kuhudhuria hafla maalum hapa Dar es Salaam kusherehekea maadimisho hayo. Hafla hiyo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 

Mwakilishi Mkazi wa FAO hapa nchini, Bw. Fred Kafeero, amethibitisha kuwa Bw.  Graziano da Silva atakuwa hapa nchini kufuatia mwaliko wa Serikali ya Tanzania. “Mkurugenzi Mkuu wa FAO atabadilishana mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda,” alisema. Bw. Graziano da Silva pia atajadili mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala mengine ya umuhimu kati ya pande hizo mbili, aliongeza. Mbali ya Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za utafiti. 

Baadae Mkurugenzi Mkuu ataenda Zanzibar ambapo, miongoni mwa mambo mengine, anategemewa kuweka jiwe la msingi katika jingo la Mradi wa Kuzalisha vifaranga vya samaki unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa KOICA.  Pia Bw. Graziano da Silva atapata fursa ya kutembelea mradi wa kilimo cha mwani na pia kuona maonesho ya bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa na wanawake wanaojihusisha na kilimo cha mwani.

Tanzania ilijiunga na FAO mwaka 1962, na mwaka 1977 FAO ilifungua ofisi zake hapa Tanzania. Katika miaka 40 ya uwepo wake, FAO imeisadia Serikali ya Tanzania katika kupanga na kutekeleza sera, mikakati na mipango ya kilimo hapa nchini. Kazi ya FAO imejikita katika kuboresha usalama wa chakula na lishe pamoja na maisha ya wakulima wadogo na hivyo kuwa chachu ya kukua kwa uchumi kupitia sekta ya kilimo. 

Posted by Editor on 14:04. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MKURUGENZI MKUU WA FAO KUZURU TANZANIA, KUFANYA MAQZUNGUMZO NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA SERIKALI, WADAU

Post a Comment

Photo Gallery

Designed by Solaranlagen | with the help of Bed In A Bag and Lawyers