MISS KIGAMBONI WAINGIA KAMBINI
Baadhi ya Warembo wanbaoshiriki shindano la Redds Miss Kigamboni City 2012 wakimsikiliza Mwalimu wao Laura Kombe aliyekuwa akiwapa maelekezo wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa ndani wa Brake Point Outdor jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya warembo 15 wanajifua kwaajili ya kuwania tajhi hilo.
(Picha na FATHER KIDEVU BLOG)
(Picha na FATHER KIDEVU BLOG)
---
Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya warembo 15 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' ambalo litafanyika Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na bado milango iko wazi kwa warembo wengine wanaotaka kuwania taji hilo ili kutoa nafasi ya kupata mwakilishi atakayefanya vyema kwenye ngazi ya kanda na taifa hapo baadaye.
"Bado hatujafunga milango, tunawakaribisha wasichana wenye sifa kujiunga ili tuweze kupata mshindi atakayepeperusha kitongoji cha Kigamboni vizuri," alisema mratibu huyo.
Alisema kuwa kampuni yake ya K & L iliyopata baraka za kuandaa shindano hilo imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa Miss Temeke mwaka 2003 kuwa ni pamoja na Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili, Doreen Kweka, Agness Goodluck, Khadija Kombo, Lina David, Aisha Mussa, Edda Silyvester, Fatina Francis na Rosemary Deogratius.
Alisema kwamba shindano hilo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine, Screen Masters, Clouds FM, Times FM na NSSF.
Taji la taifa la shindano hilo linashikiliwa na Salha Israel ambaye alitokea katika Kanda ya Ilala.