TAWLA yaendesha Semina kwa Waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa Afya ya Uzazi salama kwa Wanawake katika mchakato wa Katiba Mpya
Wakili Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake (TAWLA) akiwasilisha mada katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali iliyoandaliwa na TAWLA inayozungumzia Mabadiliko ya Katiba na haki ya Afya ya Uzazi salama inayofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es salaam hivi sasa.Moja ya mada zilizochukuwa muda mrefu kujadiliwa ni kuwa katika Mchakato wa Katiba Mpya ni vyema izungumze wazi juu ya umuhimu wa Afya ya Uzazi salama kwa Wanawake na pia mtoto wa kike atambulike kuwa ni mtu mzima akiwa na miaka 18 na pia izungumze wazi juu ya elimu ya mtoto wa kike, kuwa angalau apate elimu kufikia kidato cha nne.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Chama cha Wanasheria wanawake (TAWLA),Tike Mwambipile akizungumzia juu ya umuhimu wa Afya ya Uzazi salama kwa Wanawake kwenye jamii pia alisisitiza kuwa swala la Uzazi salama kwa Wanawake ni vyema likaangaliwa vizuri kwenye Mchakato Mzima wa Katiba Mpya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
Posted by Editor
on 23:17.
Filed under
eastafricannews,
feature,
gallery
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0