Share this Post

dailyvideo

Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania asherehekea miaka 35 ya nchi yake

Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akiongea machache kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 35,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo mabalozi kutoka sehemu mbalimbali,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo nyumbani kwa balozi huyo,jijini Dar.
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo,Pichani kati ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo,wakisherehekea hafla fupi ya  kutimiza miaka 35 ya jamhuri ya Djibout iliyofanyika jioni ya leo jijini Dar.
 Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akimpokea mgeni rasmi wa hafla hiyo,Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi alipokuwa akiwasili nyumbani kwa balozi huyo.
 Balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo  akimkaribisha Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons) mara alipokuwa akiwasili kwenye hafla hiyo.
Sir Andy Chande akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi jioni ya leo kwenye viunga vya balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akizungumza machache na machache na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi ,shoto ni Sir Andy Chande
Balozi Shamo na Mkewe wakiwa na wageni wao waalikwa waliofika kujumuika nao kwenye hafla hiyo.
Mke wa Balozi,Mariam Shamo (wa nne shoto) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwa na Mkewe Juhayna Kusaga wakifurahia jambo kwenye hafla hiyo
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi akizungumza jambo na Sir Andy Chande
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi akizungumza machache kuhusiana na hafla hiyo kwa baadhi ya wanahabari waliohudhuria ,shoto ni Sir Andy Chande.
Picha zote kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

Posted by Editor on 11:54. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania asherehekea miaka 35 ya nchi yake

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery