Share this Post

dailyvideo

MASTAA WA BONGO: Diamond msanii atumia zaidi ya Milioni 69 kujenga nyumba yake iliyopo Tegeta.


Inawezekana ukawa una taarifa kwamba Diamond Platnums ni msanii mwenye mkwanja sana hapa Tanzania kutokana na show za bei gali na nyingi anazozifanya.

Inawezekana ukawa unataarifa kwamba Diamond Platnums ndio msanii ambae yuko juu kwa sasa Tanzania, na kwamba ndio msanii aliepiga show nyingi za bei ghali mwaka jana.

siyo hayo tu… kuna uwezekano ukawa una taarifa zake nyingi tu lakini hili ninalotaka kukwambia mimi ndio kwanza unalisoma kutoka hapa.

Akiongea Exclusive na millardayo.com Platnums amekubali kuzungumzia nyumba yake anayoijenga Tegeta Dar es salaam kutokana na pesa za muziki.

Amesema “ninapopata huwa najaribu kutengeneza vibanda vyangu vinisitiri manake ninazo nyumba tofauti tofauti, nyumba ya Tegeta nimetumia milioni 69 mpaka sasa, leo wanapiga plasta nyumba imekaribia kuisha kabisa, ni ya vyumba vinne titatu ni Master, kuna jiko kubwa tu, choo cha public, studio, dining, sitting room… ni nyumba ya kisasa, kiwanja nilikinunua mwezi wa tisa 2011, nyumba nyingine ninazojenga zipo zipo ila huwa sipendi kuzizungumzia”

Habari kwa hisani ya millardayo.com   

Posted by Editor on 15:28. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MASTAA WA BONGO: Diamond msanii atumia zaidi ya Milioni 69 kujenga nyumba yake iliyopo Tegeta.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery