MATUKIO KATIKA MKUTANO WA SADC LUANDA, ANGOLA JANA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia) wakizungumza na Rais wa Zambia, Michael Santa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC uliofanyika leo Juni 1, 2012, Luanda Angola. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano huo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia katika mazungumzo kati yake na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Namibia, Hage Geigob wakati walipokutana katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, Luanda leo. Picha na PMO




