Share this Post

dailyvideo

THE MBONI TALK SHOW NDANI YA BONGO CELEBRITY


Kuanzia leo, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake.Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Mashimba.

The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi,Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa  1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).

Lakini Mboni Mashimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu;

BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?

MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?

BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?

MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni  ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa



FATILIA MAHOJIANO HAYO KWA KUBOFYA HAPA.

Posted by Editor on 09:14. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for THE MBONI TALK SHOW NDANI YA BONGO CELEBRITY

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery