Share this Post

dailyvideo

Mbunge CCM akamatwa kwa rushwa




Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary
Badwel
Neville Meena na Fidelis Butahe

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary
Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi
wa Serikali.



Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi
wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo zinaeleza kuwa Badwel
alikamatwa na maofisa wa Takukuru jana saa 9:00 alasiri katika Hoteli ya
Peacock jijini Dar es Salaam.



Badwel ambaye ni mjumbe wa Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) anadaiwa kukamatwa wakati
anapokea rushwa kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani jana.



Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa
wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho
ambapo watamfikisha mahakamani.



“Siwezi kumataja aliyekuwa akitoa
rushwa kwa sababu bado tunaendelea na upelelezi, ila mpaka sasa yuko
mahabusu na tutamfikisha mahakamani Jumatatu(kesho),” alisema Mfungo.



Alisema kuwa mbali na kumfikisha mahakamani, pia watatoa taarifa zaidi za tukio hilo kesho.
Endelea Hapa

Posted by Editor on 09:45. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Mbunge CCM akamatwa kwa rushwa

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery