NAIBU SPIKA MHE. JOB NDUGAI AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI KOREA KUSINI
Mhe. Naibu Spika, Job Ndugai,Mb akizungumza na Watanzania waishio Korea Kusini katika Chuo Kikuu cha Dongkukk wakati alipoalikwa kutoa mada MCHANGO NA NAFASI YA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI KATIKA BUNGE. Kushoto katika meza kuu ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Korea Kusini, Nd. Emmanuel Lupilya na kushoto ni Katibu wa Jumuiya hiyo Nd. Msofu.
Baadhi ya watanzani waishio Korea Kusini wakimsikiliza Mhe. Naibu Spika Ndugai,Mb alipokutana nao katika Chuo Kikuu cha Dongkukk jijini Seoul. Watanzania hao walimuomba Mhe. Naibu Spika kuwasilisha maombi yao kwa Serikali juu ya umuhimu wa kufungua Ubalozi nchini Korea Kusini kama zilivyofanya hivi karibuni nchi za Ethiopia na Kenya na hivyo kunufaika kwa kiasi kikubwa na fursa mbali mbali zinazotokana na mahusiano ya kidiplomasia ya karibu baina ya nchi hizo mbili.
Picha ya pamoja ya Watanzania waishio nchini Korea Kusini na Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai,Mb ambae aliambatana na Balozi Johan aliewahi kuwa Balozi wa Korea nchini Tanzania 2001-2004, ambae pia husaidia shughuli za visa na huduma nyinginezo kwa Wakorea wanaohitaji kwenda Tanzania.




