Share this Post

dailyvideo

Tundaman kutambulisha video yake mpya iliyomgharimu mamilioni

Pata picha kwenye video ya muziki wanaonekana Jackline Wolper, Lulu (muigizaji aliyepo mahabusu kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Steven Kanumba), Shilole, Anti Ezekiel, Diamond, Mo Racka na wengine!
Awamu hii Tundaman hataki mchezo na amefumba macho kwa gharama yoyote ile ili kupiga kioo (video) cha ukweli na nyota hao wote hapo juu wataonekana.
Kwa mujibu wa Tundaman hiyo ni video ngumu, iliyochukua muda mrefu na yenye gharama kubwa kuliko zote alizowahi kufanya.
Baada ya kusuburia kwa hamu video hiyo iliyofanywa na Adam Juma, director mwenye kazi nyingi za aina hiyo pengine kuliko wote nchini, ijumaa hii itatambulishwa rasmi.
Video imetumia muda mrefu kutokana na mchakato mzima wa kutafuta watu watakaoonekana ndani ambao wengi wao ni watu maarufu na walio busy na mambo mengi.
Video hiyo ni ya wimbo wake uitwao ‘Dem Sio’ unaomzungumzia msichana mwenye tabia (mbaya) tofauti na wasichana wengine.
Chanzo Bongo Flava Music

Posted by Editor on 09:22. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Tundaman kutambulisha video yake mpya iliyomgharimu mamilioni

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery