Share this Post

dailyvideo

UPDATES: KESI YA MAUAJI YA SWETU FUNDIKIRA KUSIKILIZWA KESHO, 4 JUNE 2012.



Hayati Swetu Fundikira
---

Imeripotiwa kuwa MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,Juni 4-8 itaanza kusikiliza kesi ya mauaji ya mtoto wa Chifu Abdallah FundikiraSwetu Fundikira, inayowakabili MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Mbweni na wenzake.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya uendeshaji wa kesi za Mahakama Kuu ambayo gazeti la Tanzania daima imeiona nakala yake, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Jaji Zainabu Mruke na jumla ya mashahidi tisa wa upande wa jamhuri watatoa ushahidi katika kesi hiyo.
Washtakiwa wengine ni MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) waJeshi la Wananchi (JWTZ) Kikosi cha Kunduchi na MT 85067Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.
Wakili wa serikali Dionisia Saiga awali alidai mahakamani hapo kuwa Januari 23, 2010 kuanzia majira ya saa 6 usiku, kuwa marehemu akiwa na wenzake wawili aliuawa na watuhumiwa hao wakati akijaribu kumuokoa dereva wake asipigwe na askari huyo.




Posted by Editor on 20:10. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for UPDATES: KESI YA MAUAJI YA SWETU FUNDIKIRA KUSIKILIZWA KESHO, 4 JUNE 2012.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery