Share this Post

dailyvideo

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa Aongoza Wajumbe Wa Kamati Kutembelea Ubalozi wa Tanzania Washington DC




  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wameanza ziara ya siku mbili Washington DC, kuanzia tarehe 2 - 4 Julai 2012. Pichani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzania Washington DC.


 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.)akifuatilia taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania Moscow, kutoka kwa mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa aliyejumuika na msafara huo akitokea  Moscow.


  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Lilly Munanka akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) kwenye ofisi za ubalozi


  Kaimu Balozi wa Tanzania Mhe. Lilly Munanka akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walioanza ziara ya siku mbili Washington DC


 Baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wakipata picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo

Posted by Editor on 14:47. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa Aongoza Wajumbe Wa Kamati Kutembelea Ubalozi wa Tanzania Washington DC

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery