Polisi Kanda Maalum Ya Jijini Dar es Salaam imewatawanya Kwa Mabomu ya Machozi Wachimba Kokoto Mjimwema Kigamboni
Baadhi ya mawe yaliyoondolewa barabarani baada ya kuwekwa na wachimba
kokoto eneo la Maweni, Kigamboni. Watu kadhaa wanaotuhumiwa kufanya
vurugu hizo wametiwa mbaroni.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa wameweka doria
katika barabara kuu ya kutoka Kigamboni kwenda Mji Mwema Dar es Salaam jana, baada ya kudhibiti vurugu za wachimba kokoto wa eneo la Maweni
ambao walifunga barabara hiyo kwa mawe kwa zaidi ya masaa natatu na
kuchoma matairi wakishinikiza kuruhusiwa kuchimba kokoto.
---
POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam jana ililazimika kufyatua risasi
na kurusha mabomu ya machozi kuwatawanya zaidi ya wakazi 3000 wa
Mjimwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam, waliofunga barabara kwa zaidi
ya saa tatu wakipinga kuondolewa eneo la machimbo kuwapisha wawekezaji.
Vurugu
hizo zilitokea saa sita mchana baada ya wananchi hao kufunga barabara
kupinga hatua ya Serikali kuwazuia kuendelea na shughuli za uchimbaji
kokoto katika eneo la Maweni.
Wananchi hao walifunga barabara kwa
kuweka mawe, magogo na kuchoma matairi barabarani hali iliyosababisha
magari kushindwa kupita na kusababisha maduka kufungwa. Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Mijimwema, Sylivester Roche alisema yeye
alifungiwa ofisini na wananchi hao tangu saa 6 mchana na baada ya hapo
walikwenda kufunga barabara. “Kama isingekuwa OCD, leo tungekufa
maana walikuja wakatufungia nikiwa na wajumbe na mwakilishi kutoka
Wilaya ya Temeke,” alisema Roche.
Alisema polisi walifika eneo
hilo majira ya mchana ambapo licha ya kuwazuia bado waliendelea kufanya
vurugu jambo ambalo liliwalazimu watumia nguvu kuwatawanya. Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime ambaye alikuwepo eneo la tukio
alisema walilazimika kutumia nguvu baada ya kuona wananchi hao wamekataa
kutii amri.
“Ukishamwona mtu unamuelekeza halafu hataki lazima umshurutishe,” alisema Misime na kuongeza;
“Mimi sikuja kupambana na wananchi nimekuja kutatua tatizo ambalo wamelianzisha wenyewe.”
Kamanda
huyo alisema hadi sasa wanawashikilia watu kadhaa kwa ajili ya
mahojiano na tathimini inafanywa kujua kiwango cha uharibifu wa mali
kilichojitokeza kutokana na vurugu hizo.
Alisema pia wataendelea
kuwasiliana na viongozi wa wizara husika ili kuona ni taratibu gani
zitumike kutatua tatizo hilo ili wananchi hao waendelee na shughuli zao. Mmoja
wa wachimbaji hao, Rajabu Zuberi alisema Serikali inatakiwa kuwapa
elimu badala ya kutumia nguvu kuwaondoa kwani baadhi yao wamechukua
mikopo kwa ajili ya shughuli hizo.
“Miaka yote tunaendesha maisha
yetu kwa kutegemea mawe, leo hii wanakuja kutufukuza kama vile sisi ni
wakimbizi,” alisema Zuberi. Wachimbaji hao zaidi ya 3,000 walisema
wamekuwa wakichimba kokoto katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20 na
kwamba maisha yao yote yanategemea kazi hiyo. “Kula kwetu
kusomesha watoto na maisha yetu yote tunategemea machimbo haya hivyo
wasituondoe kama wakimbizi,” alisema Maria Masimba.
Mkazi
mwingine Cosmas Mateo alisema hivi sasa wamezuiwa kuingia katika eneo
hilo na kwamba hata wakisafirisha mizigo yao inakamatwa. Alisema
baadhi yao walikuwa na leseni zilizotolewa na Wizara ya Nishati na
Madini ambazo walikuwa wakizipata kila mwaka, lakini baadaye zilifutwa. “Serikali
iseme ukweli kama imetuchoka….tumepewa stop order (amri) hatufanyi
chochote halafu leo hii wanakuja kutuambia tuondoke kwenye machimbo
haya,”alisema Mateo.
Wakazi hao pia walilalamikia kitendo cha
wawekezaji saba wanaoendelea na shughuli ya kuchimba kokoto katika eneo
hilo kwa kile walichodai kuwa hata hao hawana leseni.Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema alisema wao hawana nia ya kuwafukuza
wachimbaji hao wanataka kuwapeleka katika maeneo yaliyotengwa kwa
shughuli hiyo.
Alisema wachimbaji hao hawana vibali maalum na
kwamba tayari walielekezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwenda kuomba
vibali katika maeneo yaliyotengwa.
“Hawajapewa siku tatu za
kuhama…kama kungekuwa na hali hiyo kungekuwa na barua ya kuwajulisha
wananchi hao,”alisema Mjema na kuongeza kuwa:“Tunambua kwamba hiyo ndiyo ajira yao hivyo wawe wavumilivu ili tuweze kuangalia namna ya kuwasaidia kwa kuwap
Posted by Editor
on 13:36.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0