Share this Post

dailyvideo

RAY: TUNAUZA HAKI ZETU KWA SABABU HATUNA JINSI.


Ray The Greatest Mtayarishaji na muongozaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi ‘Ray the greatest’ amefunguka kwa kusema ni kweli wasanii wanauza haki zao za filamu wanazotengeneza kwa wasambazaji kutokana na hali halisi ya soko lenyewe kuwa finyu likimilikiwa na kampuni moja tu, ambayo angalau imewatoa hapo walipo tofauti na siku za nyuma walivyoanza kuigiza katika televisheni.


“Ukweli si kama tunapenda kuuza haki zetu kwa wasambazaji au wanaonunua filamu, sababu kubwa ni ukosefu wa soko la uhakika pamoja na wawekezaji kushindwa kujitokeza, lakini tuwe wakweli na kukumbuka tulikotoka tulikuwa tunaigiza katika Televisheni kwa kulipwa 40,000/ tu kundi la wasanii kibao, lakini leo hii tunamiliki kampuni na kumudu maisha yetu kwa kununua magari na vitu vingine,”anasema Ray.

Ray anasema kuwa ni jukumu la serikali kuandaa mazingira yatayoweza kushawishi wawekezaji au wadau wanaoweza kuingia katika usambazaji wa filamu, lakini jambo lingine ni taasisi za kibenki kuwadhamini kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya kutengenezea filamu na kuingia sokoni au kuuza hata nje ya nchi, hilo ndilo linaweza kuleta maslahi na kuwafanya wasanii wasiuze haki zao.Zaidi bofya hapa

Posted by Editor on 18:44. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for RAY: TUNAUZA HAKI ZETU KWA SABABU HATUNA JINSI.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery