Share this Post

dailyvideo

Makala ya leo: Fahamu maisha ya jamii hii ya sisimizi wakubwa!

 Hawa ni aina ya sisimizi wakubwa wanaonekana kama siafu lakini sio, Sisimizi huyu wa upande wa kushoto alikuwa amekuja hapa kumchukua sisimizi mwenzake ambaye amepoteza maisha.
 Hapa sisimizi huyu akiwa na majonzi makubwa anaondoka kwenda kuwachukua wenzake wapate mbepa sisimizi huyo
 Hii ni sehemu inaitwa makutano ya wadudu hawa sisimizi wakubwa ambao wana ushirikiano mkubwa sana,Hapa hukutana kubadilishana  vyakula na mambo mengine mengi.
 Kama unavyo waona hapa wote wako sehemu moja wengine wanazurula katika majani ya kijani kutafuta chakula wengine wanahakikisha kuna usalama.
 Hapa kulikuwa na Jua kali sana ambapo sisimizi huyu alipata nafasi ya kujihifadhi
 Kama alivyo binadamu pia sisimizi hawa wana uwezo wa kukumbatiana na kupeana Kisses kama wanavyo onekana sisimizi hawa wawili
 Hapa ni makao makuu ya sisimizi hawa ambapo baada ya mihangaiko yote hutulia hapa na kupumzika.
 Hii ni moja ya njia za sisimizi hawa, Njia hii ni maalum kwa ajili ya kupitishia chakula
 Wale sisiizi watoto haya ndio maeneo yao yakujiachia
 Baadhi ya hifadhi za sisimizi hao  wakati wa jua kali
 Hapa sisimizi hawa walikuwa wanacheza tuu baada ya kumaliza kazi zao za kutafuta chakula
Chini ya Mti huu ndipo sisimizi hawa hupendelea zaidi kujihifadhi maana pana kivuli muda wote.
Picha zote zimepigwa na Fredy Tony Njeje
*******

Na Fredy Tony Njeje wa This Day Magazine
Ukiwatazama Sisimizi  utagundua kuwa ni viumbe wadogo sana ambao huwezi kudhania ya kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa na ushirikiano kushinda hata binadamu.

Nimekuwa nikifanya utafiti wa kina sana juu ya wadudu hawa na hatimaye bada ya kuwachunguza sana nikaona nije kuwaletea hapa japo kitu fulani mpate pia kuwafahamu.

kwa ujumla kuna sisimizi wa aina nyingi sana, kuna wale  wadogo kabisa, wengine saizi ya kati wakubwa na wale wakubwa kabisa ambao pia ni hatari sana hasa kama utawaingilia katika makazi yao.

Mbali ya hapo sisimizi sio kama siafu ambapo siafu akikukuta popote anataka kukushambulia, sisimizi wa aina nyingi hawana muda na mtu. wenyewe kazi yao kubwa ni kutafuta chakula na kuendelea na maisha yao, Kuna sisimizi wanaoishi maporini na ambao wanaparikana katika makazi ya Binadamu. Sisimizi wanaoishi maporini mara nyingi hupenda kukaa katika makundi makundi na ushirikiano mkubwa.

Mara nyingi sana sisimizi hupendelea kufanya kila kitu kwa ushirikaino mkubwa, kama ni chakula watatafuta pamoja, kama ni kwenda kumuhifadhi mwenzao aliye kufa watabeba na kumuhifadhi pamoja, sisimizi hupata muda wa kucheza pamoja, kula pamoja na kuishi pamoja kila wanapo kuwa.

Sisimizi hawana kutengana kabisa mara zote hushirikiana, wale sisimizi wadogo huachiwa huru kucheza huku wale wakubwa wakiwa wanafanya kazi kwa bidii ili kuwatunza wadogo.

Tunatumaini ya kwamba utakuwa umejifunza kitu kutoka kwa wadudu sisimizi.

Tukutane tena Muda mwengine kwenye mambo mapya ya Mazingira ambayo yanaletwa kwenu na Fredy Tony Njeje wa This Day Magazine

Posted by Editor on 18:29. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Makala ya leo: Fahamu maisha ya jamii hii ya sisimizi wakubwa!

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery