Share this Post

dailyvideo

FFU NGOMA AFRICA BAND WAKUMBANA NA WASHABIKI WALIODATA AKILI NJINI BREMERHAVEN, UJERUMANI...!!!

 Kamanda wa FFU
 Mr.Sascha ni Personal Guard wa FFU
 Ngoma africa band in Bremerhaven
 Fans wa FFU

Klimahaus-Bremerhaven,Mjengo wa ajabu
---
FFU wa Ngoma Africa band  watembeza gwaride la kufa mtu  Ughaibuni, Bremerhaven,Ujerumani.
Katika Jumba la ajabu palikua hapatoshi
Siwengine bali ni Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU,yenye maskani yake nchini Ujerumani.
Bendi hiyo maarufu siku ya Jumatano 12.9.2012 ilijikuta ikivaana jino kwa jino tena na washabiki sugu ndani ya juma la ajabu la "Klimahaus" Arena mjini Bremerhaven,Ujerumani.
Baada ya mdundo wa ngoma africa band kupenya katika nyoyo za washabiki wa mataifa mbali mbali  walifurika katika onyesho hilo wengi wao wakiwa wenyeji wa ulaya.uwanja wa dansi ulionekana mdogo na kukawa na patashika la nguo kuchanika.
Washabiki waliodata akili walijikuta wakiperekana samba samba na muziki wa ngoma africa band, kiasi cha kuwafanya walinzi wa usalama kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kila kitu kipo salama.
Ngoma Africa band aka ffu au maarufu kwa majina mengi ya utani kama vile "Watoto wa Mbwa" "wazee wa bongo tambarare" kutoka katika kabila la "Wagagagigikoko" waliogunduliwa katika maandiko ya kitabu cha Buri Cheka watatumbuiza tena siku ya Jumamosi 15.09.2012 katika
Maonyesho ya AFRIKA-MESSE mijini Bremen,Ujerumani.
Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

Posted by Editor on 14:59. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for FFU NGOMA AFRICA BAND WAKUMBANA NA WASHABIKI WALIODATA AKILI NJINI BREMERHAVEN, UJERUMANI...!!!

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery