Share this Post

dailyvideo

JAFFARAI KUANZISHA BIASHARA YA KUOSHA MAGARI..



Msanii wa Bongo Flava Jaffarai Jaffarymz amefunguka na kusema yuko kwenye dakika za mwisho za kufungua sehemu yake ya kisasa kwa ajili ya kuosha magari (Car Wash).

Kasema hiyo car wash iko Mikocheni Dar es salaam Oil Com mkabala na hospitali ya TMJ ambapo alitumia miezi mitatu kuipata hiyo sehemu ambayo ataifungua rasmi weekend ijayo.

Mtaji alioutumia hauzidi milioni kumi za kitanzania, ni mtaji ambao muziki umechangia asilimia 70 au 80 ya pesa ambazo alianza kuzikusanya kutokana na muziki toka 2003, hiyo ni kutokana na showz pamoja na mauzo ya ringtones na pia show alizofanya Afrika Kusini hivi karibuni zimempa mavuno mazuri.

Jaffarai alisema “nilikua nataka kufanya kitu tofauti na wasanii wengine, utasikia flani ana duka, flani ana duka, flani ana duka… nitakua kwenye biashara nzuri, naweza kuhandle biashara ya kuosha magari kwa sababu watu wengi wanaonizunguka wanamagari.”

Chanzo; Jestina George Blog

Posted by Editor on 17:12. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for JAFFARAI KUANZISHA BIASHARA YA KUOSHA MAGARI..

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery