Share this Post

dailyvideo

NEWS ALERT: MCHUNGAJI MTIKILA AIBUKA KIDEDEA KATIKA KESI YA UCHOCHEZI ILIYOKUWA IKIMKABILI.


Mchungaji Christopher Mtikila akipunga mkono baada ya kutoka na ushindi katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili katika mahakama ya Kisutu jiji Dar es Salaam leo.
Ambapo amesema kwamba alikuwa anajua kwamba hakuwa na kosa na kuwa maandiko yamesema ‘isimamie imani yako’ na ndivyo alivyofanya, na kuwa ametekeleza maagizo ya Biblia na haki yake ya kuiamini na kuitetea iko katika katiba ya Jamhuri na katiba hiyo imesema ‘asiingiliwe’
Mchungaji Mtikila akinong’onezana jambo na mtu wake wa karibu mahakamani hapo wakati akisubiri hatma ya kesi yake.
Akitoka mahakamani kwa kicheko baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mchungaji Mtikila akizungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema katika nchi hii atamshangaa mtu asiyeguswa na kutetemeka katika masuala yanayomhusu Mwenyezi Mungu. Hivyo lazima tumuombee hakimu wa kesi yake na mahakimu wengine wote inapofika katika jambo linalomhusu Mungu.
Na. MO BLOG TEAM.
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa akikabiliwa na kesi ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.
Mtikila anadaiwa kati ya Januari 2009 na Aprili 17- 2010 jijini Dar es Salaam kwa nia ya uchochezi alisambaza kwa umma nyaraka za uchochezi.
Na katika Shitaka la pili, anadaiwa Aprili 16, 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka huo wa uchochezi kwa jamii.
Picha na maelezo kwa hisani ya Mo Blog

Posted by Editor on 15:46. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for NEWS ALERT: MCHUNGAJI MTIKILA AIBUKA KIDEDEA KATIKA KESI YA UCHOCHEZI ILIYOKUWA IKIMKABILI.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery