Share this Post

dailyvideo

NEWS ALERT: MSAJILI WA VYAMA ATANGAZA KUKIFUTA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NCHINI KITAKACHOCHEA VURUGU NA KUVUNJIKA KWA AMANI.



Na.MO BLOG TEAM
Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Bw. John Tendwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake ambapo amesema sasa ni mwanzo na mwisho kwa chama chochote cha siasa kujihusisha na vurugu ambazo zinapelekea kutokea kwa mauaji. Hivyo amewataka wanasiasa wote nchini kufanya siasa za busara bila vurugu ya aina yoyote. Amesema hapendi mtu afe kwa ajili ya mikutano na kutaka sasa tufikie mwisho wa mauaji.

Posted by Editor on 19:42. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

1 comments for NEWS ALERT: MSAJILI WA VYAMA ATANGAZA KUKIFUTA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NCHINI KITAKACHOCHEA VURUGU NA KUVUNJIKA KWA AMANI.

  1. Anonymous

    Jeshi la polisi ndio chanzo cha vurugu. kuna haja ya msajili wa vyama vya siasa au taasisi nyingine muhimu kuchunguza mwenendo wa jeshi la polisi na uhusiano wake na vyama vya siasa. Nguvu zinazotumiwa na polisi kuvuruga maandamano yasiyo na madhara au mikutano hata ya ndani ya vyama vya siasa haina mantiki. Hivi maandamano ukiyapangia njia na kuyawekea ulinzi unaathiri nini? mbona wanalinda mikusanyiko isiyo na tija kwa nchi kama matamasha ya burudani? kwa nini inakuwa ngumu sana kwa polisi kureason na kuchukua hatua za kitaalam kusaidia siasa za amani?

    Ni polisi hawa hawa waliovamia watu mpaka ndani ya kanisa miezi michache iliyopita. that was unthinkable.

    Sijui kama polisi wa nchi yetu wanaangalia hata TV jinsi wenzao wa nchi zilizoendelea wanavyofanya kazi zao katika mazingira ya kisiasa. au ni vile kipato chao ni kidogo hawawezi kununua TV na wanatolea hasira zao kwa wananchi wasio ha hatia.
    Si kila wakati unapaswa kutumia nguvu. Hivi kama wananchi umewaambia wasiandamane na kwamba nguvu itatumika kuwatawanya, lakini bado wakaja kwa wingi kuandamana, Polisi hawezi kufikiri vizuri hata kuona huenda katazo liko against interest za raia na walipa kodi wanye kiu juu ya jambo husika?
    kuna wakati polisi wanapaswa kurudi nyuma na kuangalia kama mbinu wanazotumia kushughulikia mambo ya kisiasa zinafanya kazi au la. otherwise kufungia vyama sio solution, kwa kuwa chama ni watu ambao wana uhuru wa kikatiba wa kuwa wanachama wa vyama vya siasa. ukifungia kimoja wataanzisha kingine au kujiunga na chama kingine. labda uvunje mfumo mzima wa siasa za vyama vingi.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery