SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA 127 WA JUMUIYA YA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI (IPU) NCHINI CANADA.
Mhe. Anna S. Makinda (Mb) Spika wa Bunge la Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania anatarajia kuongoza Ujumbe wa Waheshimiwa Wabunge Wanne
Kushiriki Mkutano na Jumuiya ya Umoja wa Mabunge Duniani Inter - parliamentary
Union (IPU) utakaofanyika mjini Qubec
nchini Canada kuanzia tarehe 21 – 26 Oktoba 2012 ikiwa ni sehemu ya kuimarisha
diplomasia ya kibunge (Parliamentary
Diplomacy).
Ujumbe huo wa Waheshimiwa
Wabunge utakaoshiriki Mkutano huo kutoka Tanzania ni pamoja na:
- Mhe. Hamad Rashid Mohamed (Mb)
- Mhe. Susan L. Lyimo, (Mb)
- Mhe. David Kafulila (Mb) na
- Mhe. Dkt. Pudenciana kikwembe (Mb)
Agenda kubwa ya Mkutano huu ni kulenga kuendeleza Mahusiano
ya Mabunge Duniani katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii sanjari na
demokrasi ya kweli inayohusu mjadala uliopewa jina la Uraia, Utambulisho na Lugha, na
Mtambuka wa Kuutamaduni katika Dunia ya Utandawazi (Citizenship, identify and linguistic and culture diversity in a
globalized world).
Pamoja na mjadala kuhusu mada hii, Wabunge katika Jumuiya
hiyo watajigawa katika kamati mbalimbali kujadili masuala mbalimbali ya kibunge
ambayo yamepewa mada zifuatazo:-
- Enforcing the Responsibility to protect the Role of Parliament in Safeguarding civilians lives
- Fair Trade and innovative financing mechanism for sustainable development
- The use of media including social Media to enhance citizen engagement and democracy
Aidha taarifa ya Jumuiya ya Umoja wa Mabunge Dunia (IPU)
kuhusu mahusiano yake na umoja wa Mataifa itatolewa kwa washiriki wa Mkutano
huo ikifuatiwa na Mijadala mingineyo saba amabayo itakuwa na maada zifuatazo:
- Mahusiano ya Nchi na nafasi ya diplomasia ya Kibunge (Multilateralism and the role of Parliamentary Diplomacy)
- Mahitaji Makubwa ya Mafuta: Nini Matarajio ya Usalama wa Nishati (Peak Oil: What prospects for energy security
- Ujengaji wa amani baada ya Migogoro (Building Peace after Conflict)
- kujenga fursa za Vijana katika uchumi wa kitandawazi (Creating Opportunities for youth in today’s global economy)
- Kinga za Kibunge: ni kwa manufaa au Mzigo? (Parliamentary immunity: benefit or burden?)
- Bunge na sheria za siasa, (Informal Panel: Parliamentary and political law)
- Warsha kuhusu nyenzo mpya za kuwezesha kupunguza matumizi ya nguvu za nuclear (Workshop on new tools to promote Nuclear disarmament).
Pamoja na mijadala hiyo ujumbe wa Tanzania Utakutana na
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Ndg. Anders
B. Johnsson na
kufanya mazungumzo ya pamoja kufuatia Tanzania kupewa heshima ya kuwa mwenyeji
wa kuandaa Semina ya Wabunge wanawake wa Jumuiya hiyo kutoka nchi za Afrika ya
mashariki, Afrika ya kati na kusini mwa Afrika.
Semina hiyo itakayofanyika Tanzania itakuwa na mada kuhusu Mwitikio
na nmana ya kuzuia ukatili dhidi ya Wanawake: kutoka Utungaji wa Sheria Husika
hadi kufika utekelezaji wake (Preventing
and Responding to violence against Women: From legislation to effective
enforcement) na itafanyika Dar – es- Salaam tarehe 5 – 7 Desemba 2012
ambapo wajumbe zaidi ya 100 kutoka nchi 15 za SADC na Africa Mashariki
watashiriki .
Sambamba na Mkutano huo, Makatibu wa Mabunge kutoka nchi
wanachama watafanya vikao vitakavyo jadili masuala mbalimbali ya kiutendaji
ambapo katibu wa Bunge Dr. Thomas D. Kashililah
atawakilishwa na Ndugu Kileo Nyambele Mkurugenizi wa Maktaba na Utafiti
wa Bunge.
Ujumbe wa Tanzania unatarajia kurejea nchini tarehe 28
Oktoba, 2012.
Imetolewa na
Idara ya Habari,
Elimu kwa umma na Uhusiano wa Kimataifa
Dar es salaam
17 Oktoba, 2012




