Share this Post

dailyvideo

Watu wauwawa Nigeria wakitoka msikitini

Kijiji cha Dogo Dawa kwenye ramaniWakuu wa Nigeria wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha wamewauwa watu kama 20 katika shambulio lilofanywa alfajiri kwenye kijiji cha Dogo Dawa katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi.







Washambuliaji walifyatua risasi na kuwapiga visu waliokuwako na tena walimuuwa mzee wa jamii nyumbani kwake.Waliouwawa wengi walikuwa wakitoka msikitini.

Afisa wa habari wa jimbo hilo, Saidu Adamu, aliiambia BBC kwamba gengi la majambazi wa jimbo hilo walifanya mauaji hayo.
Alisema shambulio hilo ni la kulipiza hatua iliyochukuliwa na wanakijiji cha Dogo Dawa ya kuunda kikosi cha wanamgambo wao wenyewe kuwatimua majambazi hao ambao wamekuwa tishio kijijini.
Chanzo BBC

Posted by Editor on 18:43. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Watu wauwawa Nigeria wakitoka msikitini

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery