Share this Post

dailyvideo

BREAKING NEWS: Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda avamiwa,ajeruhiwa vibaya kichwani

 

 Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.
Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu. Kwa hisani ya Michuzi Blog

Posted by Editor on 08:27. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for BREAKING NEWS: Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda avamiwa,ajeruhiwa vibaya kichwani

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery