TAIFA STARS YAWASILI MARRAKECH KUKIPIGA NA MOROCCO JUMAMOSI SAA 5 USIKU KWA SAA ZA BONGO
Taifa Stars imewasili leo jijini Marrakech, Morocco tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa siku ya Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia katika hoteli ya Pullman, ambayo pia ilifikia timu ya Ivory Coast ilipotua nchini humo
kucheza na Morocco. Stars imetua na kikosi cha wachezaji 21 wakati Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu watawasili leo- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana wakitokea Maputo, Msumbiji ambapo jana- Juzi 2 mwaka huu timu yao ya TP Mazembe ilicheza mechi ya Kombe la Shirikisho.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saaa 5 usiku.
Sufiani Mafoto Blog
Sufiani Mafoto Blog





