TUNATANGAZA UTALII WA NDANI: JE UNAMJUA MNYAMA TWIGA, SOMA HAPA
Twiga ni mnyama mzuri ambaye Tanzania hutumia alama yake kama urithi wa Taifa.Twiga ni mnyama mrefu kuliko wote duniani.Ana miguu mirefu,shingo ndefu sana,ulimi mrefu na pembe fupi zilizo butu.Mwili wake una mabaka yenye rangi ya kikahawia-njano na kuzungukwa na rangi ya maziwa.
Mnyama huyu anapatikana katika nyika hususan sehemu zenye migunga pamoja na mikakaya,miti ambayo huifurahia sana na ni chakula chake kikuu.Twiga hana ushindani mkubwa wa chakula na wanyama wengine kwa vile yeye hula majani ya juu nchani wakati wanyama wengine hawafikii majani hayo.
Twiga ana urefu wa kati ya mita 4.8 na 5.5 Uzito wake ni kati ya kilo 700 na 1500.Twiga jike ana rangi ng'avu zaidi kuliko dume.Hii inaweza kuwa ni maumbile ya kuwavutia Twiga dume.Dume ni mkubwa na mzito kuliko jike.
ENDELEA KUSOMA BOFYA HAPA>>>
TUSHIRIKIANE KUWALINDA WANYAMA NA KUYALINDA





