Share this Post

dailyvideo

DIAMOND PLATNUMZ AVUNJA UKIMYA NI BAADA YA NGOMA YAKE YA NUMBER ONE REMIX KUSHIKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA TRACE TV , AFRICA 10

Jana mida ya saa Tano usiku ndani ya Moja ya Tv kubwa za Muziki Afrika iendayo kwa Jina la Trace Tv kulikuwa na African 10, yaani ngoma 10 kali sana zinazotamba Afrika kwa sasa, ambapo wale wanamuziki wakubwa wote kama Psquare, Dovido, J Martins, wakali kutoka Afrika Kusini na mataifa mengine toka Barani Afrika hushindanishwa hapo.

Hata Hivyo baada ya count down yote kupita ngoma ya kumi mpaka ya tisa zilishikwa na wasanii wakali na wakubwa pekee kutoka pande zengine za afrika na si Afrika mashariki.

Na Mwishoni kabisa mambo yalibadilika Ghafla na kushangaza watazamaji wengi pale ambapo Ngoma ya Number One Remix yake msanii Diamond aliyomshirikisha mkali Dovido  ilivyo pigwa na kushika nafasi ya kwanza.

Kitu ambacho kimedhihilisha ya kwamba Afrika Mashariki Hususani Tanzania ni wakali katika Muziki, kwa maana kuna ngoma ya Dovido ameiachia Juzi tuu inaitwa Eye ambayo kwa sasa inashika nafasi ya Tatu, huku wakina P square wakiwa bado huko mkiani.

Kwa ujumla Kijana Diamond anastahili Pongezi za aina yake na kwamba wanamuziki wengine wa Tanzania wanatakiwa kuiga Mfano huu kwenda 'Level Zengine' na si kulidhika tuu kwa hapa hapa nchini.

Tazama hapa baadhi ya picha za wimbo huo hapa chini na itazame ngoma hiyo hapa.
 
Endelea kuangalia chini kuona video
Picha na Habari na This Day Magazine


VIDEO


Posted by Editor on 13:13. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for DIAMOND PLATNUMZ AVUNJA UKIMYA NI BAADA YA NGOMA YAKE YA NUMBER ONE REMIX KUSHIKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA TRACE TV , AFRICA 10

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery