Share this Post

dailyvideo

DIAMOND PLATNUMZ TENA: AFANYA KOLABO NA WASANII WAKALI NIGERIA AKIWEMO IYANA NA WAJE.


Baada ya nyimbo zake kufanya vizuri sana katika nchi za Afrika Mashariki, Diamond Platnumz ameonekana kukubalika na nchi za Afrika Magharibi. Habari nzuri ni kwamba

Diamond amepata shavu la kushirikishwa katika wimbo wa mwandadada Waje. Waje ni msanii anaefahamika sana kwao Nigeria na moja kati ya wimbo uliyomtambulisha sana ni ule aliyoshirikishwa na P-square ulijulikana kama Do Me (2008).

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Waje aliandika ujumbe huu kmhusu Diamond, ”Met this amazing brother yesterday, humble nd such an inspiration,his work ethic is super. #africanlegendsmakingmusic @diamondplatnumz the talent eh. Thanks so much for this honour”

Diamond aliondoka Tanzania wiki ijayo kwenda Nigeria ambapo anatarajia kufanya kolabo na wasanii mbalimbali kutoka Nigeria na Ghana. Kolabo ya My Number One aliyofanya na Davido ndio imemtambulisha sana Afrika Magharibi.

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Posted by Editor on 12:55. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for DIAMOND PLATNUMZ TENA: AFANYA KOLABO NA WASANII WAKALI NIGERIA AKIWEMO IYANA NA WAJE.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery