Share this Post

dailyvideo

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU MUHIDINI GURUMO


Maalim Muhidin Gurumo enzi za uhai wake. 

Amezaliwa mkoa wa Pwani wilaya ya Kisarawe 1940. Elimu ya Msingi alisoma katika  Shule ya Pugu kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu, mwaka 1956, mjomba wake aliamua kumuamishia  Dar es Salaam ambako alisoma zaidi elimu ya dini 'Kuran', Mtaa wa Lindi, Ilala.Safari yake ya muziki ilianza rasmi mnamo mwaka 1967 alipojiunga na bendi ya Nuta kabla haijabadilishwa jina na kuitwa  Juwata, baadaye Ottu Jazz.

Mwaka 1978 aliamia Mlimani Park Orchestra na mwaka 1985 alijiunga na  Bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS- Ndekule)  lakini siku zote maisha yake yamekuwa Msondo ambayo ndiyo bendi iliyopitia majina ya Nuta, Juwata na Ottu.

Tangu miaka ya 1960 kama ungethubutu kutamka humjui Gurumo, ungeonekana mshamba ambaye tasnia ya muziki umeipa kisogo,alikuwa staa mkubwa sana wa muziki kipindi hicho ingawa jina  lake limebaki juu kuanzia nyakati hizo mpaka sasa.

Ni kamanda hodari, aliyeifanya Bendi ya Msondo ‘Msondo Ngoma’ ipate heshima kubwa mpaka ikaitwa Baba ya Muziki Tanzania. Tungo zake nyingi ni lulu ambayo haitafutika kamwe. Kinachoumiza kwa sasa ni kuona Gurumo hawezi tena kusimama jukwaani.Mzee huyo ndiye aliyeivusha Msondo  kupitia majina ya Nuta, Juwata,  na Ottu, ikiwa inamilikiwa na Chama cha Wafanyakazi.


Itambulike kuwa yeye akiwa na wenzake kama marehemu Shaaban Mhoja Kishiwa  maarufu kama ‘TX Moshi William’, Saidi Mabera, marehemu Suleiman Mbwembwe, Othuman Momba, Joseph Maina na wengineo, ndiyo waliounganisha nguvu na kuimiliki, baada ya chama cha wafanyakazi kujiondoa katika uendeshaji wa bendi.


Posted by Editor on 12:33. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for HISTORIA FUPI YA MAREHEMU MUHIDINI GURUMO

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery