Friday, 30 May 2014

BREAKING NEWS: MAUAJI YA KUTISHA GEITA MWANAMKE ATENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI.

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI 
Na Mwandishi wetu
Mwanamke mmoja ameuawa kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali za Mwili wake kwa kudhaniwa kuwa anaimani za Kishirikina, Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Lushiku Tenganija  Sono Msukuma aliyekuwa na Umri wa Miaka 59 wa kitongoji cha Senga kata ya Bugando Mkoani Geita ameuawa na mwili kuonekana muda wa Saa moja asubuhi  ukiwa kwenye barabara ya mtaa umbali wa mita kama mia tatu kutoka nyumbani alipokuwa akiishi Marehemu pamoja na wajukuu zake watatu.

Maremu amekatwa shingo kabisa na kutenganishwa na Mwili, mkono wa kushoto na kulia pamoja na bega la kulia. Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Joel Saanane (42) amethibitisha kutokea kwa Tukio hilo na kudai kuwa msako mkali unaendelea dhidi ya wauaji hao.

Na Geita yetu Blog.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

Sample Text