EAST AFRICAN NEWS

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI LA BOMBA LA MAFUTA GHAFI, WAFUNGUA KITUO CHA PAMOJA CHA HUDUMA ZA MPAKANI MJINI MUTUKULA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Y...

10 Nov 2017 | 0 comments | Read more

WATANZANIA WANG'ARA SHINDANO LA MWANDISHI BORA WA SAYANSI NA KILIMO AFRIKA

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwand...

29 Sep 2017 | 0 comments | Read more
ENTERTAINMENT NEWS

WAZIRI MWAKYEMBE AUDHURIA TAMASHA LA JAMAFEST NCHINI UGANDA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ugand...

14 Sep 2017 | 0 comments| Read more

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI (TASUBA) PAMOJA NA SHORT STATURE OF KENYA ZIKIONYESHA MAIGIZO TAMASHA LA JAMAFEST

 Kikundi cha burudani ya Uchekeshaji kutoka nchini Kenya maarufu kama Short Stature Society of Kenya kikitoa igizo lake la ku...

14 Sep 2017 | 0 comments| Read more

DKT.MWAKYEMBE AMEWAPONGEZA WAJASIRIAMALI WA TANZANIA KWA KUSHIRIKI TAMASHA LA JAMAFEST KAMPALA, UGANDA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia ngoma ya kiutamaduni iliy...

14 Sep 2017 | 0 comments| Read more

WORLD NEWS

TECHNOLOGY

CONGRESS TO SMART DEVICE MAKERS: YOUR SECURITY SUCKS

Four senators propose the "Internet of Things Cybersecurity Improvement Act,"...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

HUAWEI CAME REALLY CLOSE TO SELLING AS MANY PHONES AS APPLE

Apple sold 41 million iPhones in the second quarter, while Huawei's shipments were a...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

SECRET SERVICE WILL REPORTEDLY TEST DRONE FOR TRUMP SECURITY

The Secret Service is looking at whether unmanned aerial vehicles could be use...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

WHAT APPLE'S EARNINGS TELL US ABOUT THE IPHONE 8

The iPhone 7 and 7 Plus may see it's future sibling sooner than many expected.  S...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more
CELEBRITIES NEWS

JOCKTAN MAKEKE KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADANI NCHINI NIGERIA

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan...

09 Sep 2017 | 0 comments| Read more

IMPRESSIVE! BEYONCE LOOKS SLENDER IN LOW-CUT DRESS ON SUSHI DATE IN LA WITH JAY Z

Crazy in love: Beyonce looked absolutely fabulous on a sushi date night with husband Jay Z on Wednesday ...

04 Aug 2017 | 0 comments| Read more

BLOODIED JESSICA BIEL SIZZLES IN STEAMY SEX SCENE WITH HER HUNKY ONSCREEN HUSBAND

Bloody: The gimmick of the show is figuring out why this mother and wife decided to stab a man to death in the first place ...

03 Aug 2017 | 0 comments| Read more

Share this Post

SPORTS NEWS

JOSEPH KIMWAGA KUKAA NJE MIEZI MINNE BAADA YA UPASUAJI WA GOTI

WINGA wa Klabu ya Azam FC Joseph Kimwaga akiwa katika chumba cha matibabu katika Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini ...

06 Sep 2017 | Read more
HEALTH NEWS

PAMOJA NA UNENE LAKINI HAWEZI ACHA KULA

The Brazilian boy, known only as Misael, was born a healthy 6lb 6oz (2.9kg) But every month since, has gained 6lb (3kg), meaning he str...

29 Sep 2014 | Read more
TOP TEN

Top 10 ‘Breaking Bad’ Moments

Ursula Coyote / AMC 10. The ricin’s fate is revealed For all its discussion over the course of the series, ricin had never been ...

08 May 2014 | Read more
FACTS

WACHINA NOMA SANA

 Ukisikia Wachina balaa sasa hii ni moja wapo, Kiwanda Kimojawapo cha China kijulikanacho kwa jina la LandWind kimeibuka na Kutengene...

25 Nov 2014 | Read more
ENVIRONMENT NEWS

A CLIMATE CHANGE INSPIRED PROJECT LAUNCHES IN DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399 ...

04 Aug 2017 | Read more
FASHION

MH. CATHERINE MAGIGE AZINDUA RASMI DUKA LA ZURII HOUSE OF BEAUTY

. MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige  leo amezindua rasmi  duka ...

12 Jan 2015 | Read more
HISTORY

MAKALA FUPI: Mwanamke aliyehukumiwa kifo Sudan ajifungua

Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuas...

28 May 2014 | Read more
TRAGEDY NEWS

JOCKTAN MAKEKE KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADANI NCHINI NIGERIA

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan...

09 Sep 2017 | Read more

dailyvideo

HATARI : Boko Haram yauwa watu wengine 300


Kundi la Boko Haram nchini Nigeria limeuwa watu wengine zaidi ya 300 kaskazini mwa nchi, na nchi zaidi zenye nguvu duniani, zikiwemo Marekani na China zimejiunga na juhudi za kuwatafuta wasichana waliochukuliwa mateka.
Mojawap ya maeneo yaliyoshambuliwa na Boko Haram katika mji wa Maiduguri Mojawap ya maeneo yaliyoshambuliwa na Boko Haram katika mji wa Maiduguri
Juhudi hizo zinafanyika wakati ambapo kundi hilo pia limewaua mamia ya watu wengine kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, wiki hii. Huku kukiwa na hasira kutoka duniani kote, Marekani, Uingereza na Ufaransa, zinapeleka timu za wataalamu kuisaidia Nigeria katika juhudi za kuwakomboa wasichana hao.
China imeahidi kutoa taarifa zozote muhimu zitakazopatikana kwenye picha za satelaiti zake na idara za kijasusi kwa serikali ya Nigeria. Rais Barack Obama wa Marekani, amesema kitendo hicho kinasikitisha na kwamba timu ya watalamu wa kijeshi imepelekwa Nigeria kutoa msaada.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amelaani vikali utekaji nyara huo uliofanywa na Boko Haram, Aprili 14.
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria
Cameron amesema timu ndogo ya wataalamu wa mipango na uratibu itakwenda nchini Nigeria mapema iwezekanavyo.
Jana (07.05.2014) Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan ameukubali msaada huo uliotolewa na mataifa hayo ya Magharibi. Serikali ya Rais Jonathan imekosolewa vikali na wanaharakati pamoja na wazazi wa wasichana hao, jinsi inavyolishughulikia suala hilo. Jana polisi wa Nigeria waliahidi kutoa Dola laki tatu kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana wanafunzi hao wa kike.
Watu 300 wauawa
Hata hivyo, wakati juhudi za kuwaokoa wasichana hao zikiendelea, imeripotiwa kuwa wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu wamewaua watu 300 nchini Nigeria kwenye mji ulioko katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon. Kundi la Boko Haram limesema kuwa liliwafyatulia raia risasi kiholela wakati wakijaribu kuukimbia moto uliowashwa kwa makusudi kwenye mji wa Gamboru Ngala, katika jimbo la Borno.
Inaaminika kuwa watu hao waliokuwa na silaha, walilivamia eneo hilo na kulichoma moto. Seneta wa eneo hilo, Ahmed Zannah, amesema kiasi watu 300 wameuawa katika shambulio hilo lililotokea baada ya wanajeshi wa serikali kuondolewa katika eneo hilo na kupelekwa karibu na mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri, katika harakati za kuwakomboa wasichana wanaoshikiliwa mateka.
Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau
Zannah amesema hali hiyo imesababisha eneo la Gamboru Ngala kutokuwa na ulinzi wa kutosha. Jeshi la Cameroon limeimarisha ulinzi kwenye eneo la Fotokol, lililoko kwenye mpaka na Nigeria.
Siku ya Jumanne, wasichana wengine wanane walitekwa nyara na watu wenye silaha katika kijiji cha Warabe, kaskazini-mashariki mwa Nigeria. Akizungumza katika mkanda wa video siku ya Jumatatu, kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alisema wasichana hao wanashikiliwa kama watumwa kwa ajili ya kuuzwa.
Juhudi za kuwakomboa wasichana hao zinafanyika wakati ambapo Kongamano la Kimataifa kuhusu Uchumi wa Afrika, likiwa limefunguliwa rasmi jana, kwenye mji mkuu wa Nigeria, Abuja. Rais Jonathan amesema ana matumaini kwamba kongamano hilo litaonyesha maendeleo ya uchumi wa Nigeria.
Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/AFPE
Mhariri: Gakuba Daniel
DW Swahili

Posted by Editor on 15:09. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for HATARI : Boko Haram yauwa watu wengine 300

Post a Comment

Photo Gallery

Designed by Solaranlagen | with the help of Bed In A Bag and Lawyers