JITAMBUE SASA: USIKUBALI KUACHIKA UKIWA KWENYE UCHUMBA
UJANA una mambo mengi lakini vijana wa zama hizi tumezidisha. Matukio
ndani ya uhusiano ni mengi zaidi ya wakati uliopita. Kukutana na
wanandoa wanaoachana baada ya miaka miwili tu ni jambo la kawaida siku
hizi.
Si ajabu tena kusikia msichana amechumbiwa na amevalishwa
pete kabisa lakini baada ya siku kadhaa anaachwa. Hii ni aibu! Utakuta
msichana hadi anaingia kwenye ndoa, ameshavaa pete za uchumba kutoka kwa
wanaume hata wanne tofauti!
Ni mabadiliko mabaya lakini
yanayosababishwa na mfumo mpya wa maisha ya sasa. Ndugu zangu, lazima
tujifunze mambo muhimu ya kufanya ili uhusiano uwe wenye maana.
Vilio
vya wasichana wengi ni kuhusu kuvalishwa pete au kudumu kwenye uchumba
kwa muda mrefu, lakini ghafla mwanaume anamuacha na kuanzisha uhusiano
na mwingine.
Hebu tujiulize; ni tamaa za
wanaume hao au tatizo lipo kwa wanawake wenyewe? Dada zangu, naomba
mfahamu kuwa, wakati mwingine ninyi ndiyo husababisha matatizo na
hatimaye kuachwa.
Je, nini cha kufanya? Hapa nitakupa mambo muhimu ya
kukaa nayo mbali ili uweze kuingia kwenye hatua inayofuata – ndoa.
Karibuni darasani.
PATA UHONDO ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
