Wednesday, 28 May 2014

RACHEL HAULE MSANII WA BONGO MOVIE KUAGWA LEADERS CLUB NA KUZIKWA KESHO.

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Steve Nyerere akijadili jambo na wasanii wenzake
Msanii wa filamu Rachel Haule aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam anatarajiwa kuagwa siku kesho Alhamis katika viwanja vya Leaders Club na kuzikwa siku hiyohiyo katika makaburi Kinondoni.
Akizungumza na mtandao huu jana mwenyekiti wa bongomovie Steve Nyerere amesema kuwa bado wapo kwenye mikakati ya kukusanya michango itakayosaidia shughuli hiyo.
“Tulikuwa tunachangishana pesa ili kuwezesha suala la msiba,tunashukuru Mungu mambo yameenda salama, suala la kuaga ,tutaaga siku ya alhamisi pale Leaders na baada ya hapo tutaelekea katika makaburi ya Kinondoni kwenda kumzika ndugu yetu, “alisema.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

Sample Text