NGOMA ZA BAIKOKO, KANGAMOKO NA VIGODORO ZA PIGWA MARUFUKU DAR ES SALAAM.
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
Jeshi la
polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma za
kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika nyakati za usiku kwenye maeneo
mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana makundi ya
kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia
kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo
wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu,
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema
‘ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku’
Kamanda Kova
anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo vya
kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya mia moja
ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu
vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama
‘vigodoro’ pamoja ‘baikoko’ na sasa jeshi la polisi limetoa onyo kali
kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia sasa.
Posted by Editor
on 14:47.
Filed under
entertainmentnews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0