Share this Post

dailyvideo

VIDEO: Viongozi mbalimbali waunga mkono mashindano ya Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mhe. Juma Nkamia (Naibu Waziri wa Habari na Michezo), Mhe. Jenista Mhagama (Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Mhe. Halima Mdee (Mbunge wa Kawe), Mhe. Martha Mlata (Mbunge Viti Maalum) wametokea katika video ya pamoja wakiunga mkono na kupongeza mashindano ya Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula yanayoendelea hivi sasa. 

"Ukichukua mazingira ambayo wakina mama wengi wanaishi, vijana wengi wanayoishi, wakati mwingine unaona kwamba wanapoteza mwelekeo, lakini wanapopata nafasi ya kushiriki, kwa mfano kwenye Maisha Plus, wanapata pia nafasi nyingine ya kujifunza mambo mapya na utamaduni halisi wa taifa letu la kitanzania." Anasikika Mhe. Jenista Mhagama.

Mashindano hayo ambayo yanafanyika katika kijiji cha siri cha Maisha Plus yanawakutanisha wakulima wanawake wapatao 20 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na vijana 16 walioingia fainali kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda.

Kumbuka
Fainali za mashindano hayo zinatarajiwa kufanyika tarehe 18/05/2014 ambapo mshindi kwa upande wa Mama Shujaa wa Chakula atajishindia zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 25 (Milioni 5 katika hizi ziliongezwa na Mhe. Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi siku alipowakaribisha Mama Shujaa kijijini INGIA HAPA KUONA TUKIO LA AWALI LA UZINDUZI na mshindi kwa upande wa vijana atajishindia Tzshs. Milioni 25 ya mradi atakaopendekeza.

Fainali hizi zitaonyeshwa LIVE na TBC1 siku ya Jumapili tarehe 18/05/2014 kuanzia saa nne usiku.

MAISHA PLUS/MAISHA SHUJAA WA CHAKULA


Posted by Editor on 18:33. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for VIDEO: Viongozi mbalimbali waunga mkono mashindano ya Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery