Share this Post

dailyvideo

WACHEZAJI WAWILI WA UJERUMANI WATAKAOCHEZA KOMBE LA DUNIA WAPATA AJALIWachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia
Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Ujerumani itakayoshiriki kombe la dunia hukop Brazil mwezi ujao
wamenusurika baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakiwa Italia.
Benedikt Hoewedes na Julian Draxler walikuwa ndani ya magari tofauti katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya magari ya Mercedes .
Moja ya magari yaliyohusika iliwagonga wapita njia wawili karibu na makahawa wanakoiswahi timu ya taifa ya Ujerumani.
Mwathiriwa moja anauguza majeraha mabaya .

Wachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia
Ajali ya pili ilimhusisha dereva wa mbio za magari ya langalanga wa Mercedes , Nico Rosberg.
Hoewedes na Draxler ni wachezaji wa timu ya Schalke 04 walioitwa katika timu ya taifa.
Wenyeji wao kampuni ya Mercedes-Benz imetoa taarifa kusema kuwa itashirikiana na maafisa wa polisi kutathmini kilichotokea .
Timu hiyo ya Ujerumani inatarajiwa kuendelea na kambi ya mazoezi katika mji wa Tyrol Kusini mwa Italia hadi juni mosi. .

BBC SWAHILI

Posted by Editor on 10:54. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for WACHEZAJI WAWILI WA UJERUMANI WATAKAOCHEZA KOMBE LA DUNIA WAPATA AJALI

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery