Share this Post

dailyvideo

MAHUSIANO: ‘I AM SORRY DEAR’ IAMBATANE NA MABADILIKO LAA SIVYO…! INGIA HAPA


Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
Wiki hii kama kawaida nazungumzia mada inayogusa maisha yetu ya kimapenzi, si unajua bila mapenzi hakuna maisha! Huo ndiyo ukweli, huwezi kuishi kama jiwe au mti. Raha ya maisha ni kuwa na mpenzi wa kumpenda na yeye akakupenda kiukweli na siyo kuigiza kama ilivyo kwa baadhi ya watu.

Kwa wale walio katika mapenzi matamu na ya kweli watakubaliana na mimi kuwa mapenzi yenye amani na masikilizano ni kama ‘kapepo’ kadogo ndani ya ulimwengu huu mkubwa uliojaa vituko!
Wakati wengine wakiishi kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wanaoishi na wapenzi wao huku mioyo yao ikiwa imesinyaa! Kila siku ni karaha na vituko vya makusudi kutoka kwa wapenzi wao japo wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote.


Kila siku ni maumivu na simanzi ya moyo isiyojulikana hatima yake.
Lakini pamoja na karaha, vituko na dharau zinazofanywa na wale tuwapendao, bado kuna ambao wamejaaliwa mioyo ya uvumilivu. Hawa ni wale wanaoamini ule msemo usemao, subira yavuta heri. Yaani wanaamini ipo siku wapenzi wao watabadilika na maisha yatakuwa matamu.

Ni kweli kuna wanaofanikiwa katika hili lakini wapo ambao uvumilivu wao unapitiliza. Ndugu zangu, kila kitu kina kikomo, kama umevumilia kwa muda mrefu lakini ukaona hakuna mabadiliko, uamuzi sahihi ni ‘kusitisha safari’.

Kusoma zaidi Bofya hapa>>>>>

GPL


Posted by Editor on 14:33. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MAHUSIANO: ‘I AM SORRY DEAR’ IAMBATANE NA MABADILIKO LAA SIVYO…! INGIA HAPA

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery