Share this Post

dailyvideo

Previous messageNext messageBack to messages RUBY DEE, Mwigizaji mkongwe na “CIVIL RIGHTS ACTIVIST” Afariki Dunia.‏

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399








Ruby DEE, mmoja wa waigizaji wa muda mrefu mjini Hollywood na Broadway alipatwa na mauti siku ya jumatano usiku tarehe 11 akiwa na umri wa miaka 91. Ruby alikuwa nyumbani kwake “New Rochelle, NY” … akizungukwa na familia yake wakati mauti yanamkumba kulingana na ripoti familia yake. Ruby alikuwa pioneer kwa “African-American Women” mjini Hollywood na alijipatia umaarufu mkubwa kwenye filamu aliyoifanya miaka ya 1960 “A Raisin in the Sun” na filamu ya Director  Spike Lee “Do the Right Thing” na “Jungle Fever.” na vile vile Filamu iliyochukua budget kubwa ya Hollywood ni “American Gangster” ambayo aliigiza kama mama yake ‘Denzel Washington’.


Ruby alikuwa mshairi na screenwriter ambae alishawahi kujishindia Grammy Awards na Emmy Awards na kupokea National Medal of Arts na Kennedy Center Honors. Marehemu RUBY DEE na mumewe ambaye nae ni marehemu kwa sasa  Ossie Davis ambao walikuwa pia wagombea uhuru wa weusi huko nchini Marekani wakiwa pamoja na mwanaharakati ‘Martin Luther King Jr’ na ‘Malcolm X’. R.I.P

Posted by Editor on 19:01. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Previous messageNext messageBack to messages RUBY DEE, Mwigizaji mkongwe na “CIVIL RIGHTS ACTIVIST” Afariki Dunia.‏

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery