Rais Kikwete atua Malabo, Equtorial Guinea, kuhudhuria Mkutano wa 23 wa Umoja wa Afrika
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewasili mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo jana Juni 24, 2014
kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa –African Union (AU).
Akiwa
Malabo, Mheshimiwa Rais Kikwete pia atakuwa Mwenyekiti wa kikao cha
wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachojadili mazingira. Rais Kikwete na
ujumbe wake anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki.


Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Equatorial Guinea Mhe
Vicente Ehate Tomi alipowasili katika katika uwanja wa ndege wa
Malabo, Equatorial Guinea, jana Juni 24, 2014.(PICHA NA IKULU).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, jana Juni 24, 2014.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM.
