Share this Post

dailyvideo

KUWAONA TAIFA STARS DHIDI YA THE MAMBAS(MSUMBIJI) KIINGILIO BUKU 7 TU

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kiingilio cha chini cha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars)
na Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kitakuwa sh. 7,000.
Tiketi zinapatikana kwa mfumo wa elektroniki kupitia M-PESA.
Kiingilio hicho kwa ajili ya viti vya rangi ya rangi ya chungwa, kijani na
bluu. Viingilio katika maeneo mengine vitatangazwa baadaye.
Mshabiki ili apate tiketi anatakiwa kutumia M-PESA kwa
kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, ingiza namba ya kampuni 173399 kisha weka 7000
kwenye namba ya kumbukumbu ya malipo, na weka 7000 kama kiasi cha bei ya tiketi
na mwisho weka namba yao ya siri.


Baada ya hapo utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya
MaxMalipo kwa ajili ya kuchukulia tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo
yako.
Vituo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa
wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata
Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illutions (Millennium Tower na
Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na
Upanga).
Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to
Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station
(Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na
Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na
ofisi za TFF (PPF Tower). 

Posted by Editor on 09:38. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for KUWAONA TAIFA STARS DHIDI YA THE MAMBAS(MSUMBIJI) KIINGILIO BUKU 7 TU

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery