Share this Post

dailyvideo

SOMO LA BURE KABISA: MAKUNDI MATATU YA MAGONJWA YA NGONO

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399


Magonjwa ya kuambukizana kupitia kufanya ngono yaani kwa  Kiingereza  yanaitwa  Sexually Transmitted Infections (STI) yamegawanyika katika makundi matatu.
Maambukizo hutokea pale majimaji ya mwili kama vile mate, damu, manii, majimaji ya ukeni na kadhalika ya mtu ambaye tayari ameambukizwa, yatatangamana na ya mtu ambaye hajaambukizwa.
Kuna  aina nyingi ya magonjwa hayo ya STI  na yamegawanywa katika makundi makuu matatu kama ifuatavyo:

1. Magonjwa yenye dalili za kutokwa na usaha au majimaji sehemu za siri (ukeni na uumeni) ambayo ni kisonono, trikomonas na kandida.
2. Magonjwa yenye dalili za kutokwa na vidonda sehemu za siri ambayo ni kaswende, pangusa na malengelenge.
3. Magonjwa yenye dalili za kutokwa na uvimbe sehemu hizo nyeti ambayo ni mitoki, lakini pia pangusa na malengelenge.
Mgonjwa yeyote anaweza kuwa na zaidi ya ugonjwa mmoja wa ngono kwa wakati mmoja.
Kujitokeza kwa dalili za ugonjwa utokanao na kufanya ngono zembe  hutegemea aina ya ugonjwa, jinsi na kinga ya mwili iliyopo kwenye mwili wa mgonjwa.

Asilimia 10-15 ya wanaume na asilimia 60-70 ya wanawake  wenye kisonono hawaonyeshi  dalili yoyote, hivyo basi, ni muhimu kijana unapoelezwa na mwenzi wako uliyefanyanaye tendo la kujamiiana kwamba ameambukizwa ugonjwa wa ngono usisite kwenda hospitali kupimwa na ukigundulika upewe matibabu.
Dalili za magonjwa ya ngono:
Dalili za magonjwa ya ngono kwa wanawake zipo nyingi kama vile kusikia maumivu chini ya kitovu, kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya sehemu za siri au kuwashwa sehemu hizo za siri.
Wagonjwa pia wanaweza kupata vidonda na vipele sehemu za siri, mdomoni na sehemu nyingine za mwili au kusikia maumivu wakati wa kujamiiana, kuvimba mitoki, kuota sundosundo sehemu za siri na mgonjwa kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na muwasho au maumivu.

Dalili kwa wanaume:
Mgonjwa atasikia maumivu makali sehemu za siri wakati wa kukojoa, atatokwa na usaha au vidonda sehemu za siri au sehemu za mdomoni, atavimba mitoki au atapata malengelenge au kuota sundosundo ambayo kitaalamu huitwa warts sehemu za siri.
NINI HUSABABISHA?
Kuna sababu nyingi za mtu kuugua magonjwa haya ya ngono kama vile mtu  kujamiiana bila kutumia kondomu, wanawake au wanaume kujihusisha na ukahaba au kujamiiana huku ukiwa umelewa, hivyo kutokuwa makini na hujikuta wakipata ugonjwa wa zinaa kutokana na uzembe wa kuwa na wapenzi wengi na kujamiiana bila kutumia kondomu, kunyonyana sehemu za siri huku wakijua au bila kujua kuwa vimelea vya magonjwa ya ngono vinapatikana kwenye majimaji ya sehemu hizo.
Wengine hupata maradhi haya kutokana na vitendo vya kunyonyana ndimi bila kujua kuwa baadhi ya vimelea vya magonjwa ya ngono hupatikana mdomoni.
Jambo la kusisitiza hapa ni kwamba kisonono, kaswende na Virusi Vya Ukimwi mtu huweza kuvipata kwa kunyonyana ndimi hasa kama mmojawapo ana maambukizi na mmoja ana michubuko sehemu yoyote mdomoni.
Lakini wasichana hupata maambukizi kutokana na baadhi yao kushindwa kuwashawishi vijana wakiume kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa sababu uoga wa kuachwa, na wengine ni kutokana na tamaa ya kupata pesa pamoja na vitu vya thamani kama simu za mikononi, magari kutoka kwa watu wanaofanya nao ngono zembe.
Itaendelea wiki ijayo. GPL

Posted by Editor on 10:03. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for SOMO LA BURE KABISA: MAKUNDI MATATU YA MAGONJWA YA NGONO

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery