Share this Post

dailyvideo

SKYLIGHT BAND NI MOTO

Pichani Kutoka kushoto ni Bella Kombo akiongoza mashambulizi ya jukwaa akipewa sapoti na Digna Mbepera(katikati) na kwa mbaliiiii ni Aneth kushaba.
Kama kawaida yetu inapofika mwishoni mwa juma yaani Ijumaa huwa inakuwa ni siku ya furaha na kubadilishana mawazo, kupunguza stress za kazini.....paleee Thai Village Masaki.Kwenye Jukwaa Bendi yako matata na inayotikisa Tanzania na Jiji la Dar Skylight Band wanakuwa wanakupa burudani ya nguvu na iliyoenda shule.Karibu leo kuanzia saa 3 kamili usiku upate zile Afropop, Zouk, Lingala,Sebene, Reggae, Naija Flava na zingine kibao!
Aneth Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.

Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.

Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village

Anaitwa Hashimu Donode mkali wao akizipiga zile vocal kaliiii na tamuuu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village

Wanamwita tamu ya warembo au Sukari ya warembo si mwingine ni Sam Mapenzi akizipiga zile Vocal lainiii za taratibu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village

Le Meneja Her Self Aneth Kushaba AK 47 akiongoza Skylight Divas kuporomosha burudani ya nguvuuuu ndani ya Thai Village,Usikose raha hizi leo.

Muziki ni hisia na hapa ndicho anachokifanya Aneth Kushaba hebu mtazame anavyoimba kwa hisia kali na Vitendo ili kuwapa raha mashabiki wake huku akipewa sapoti kwa mbaliiii na Digna Mbepera(katikati) na Bela Kombo wa mwisho kushoto.

Majembeeee(vijana wa kazi)wakilishambulia Jukwaa vilivyo

Mikono kichwaniii,ahhh ahhhh majembe ya Skylight wakishambulia jukwaa kwa nguvuuuu

Joniko Flower baba ya congo akiongoza kushambulia huku akipewa sapoti na Sony Masamba(katikati) pamoja na Sam Mapenzi.

Mtia ladhaa mahiri wa Skylight akiwa anasahangaa kupata Ukodak kutoka kwa mpiga picha wetu,Huku mpiga drums Idrisa akichunguliaaa kwa mbaliiiii

Huyu jamaa ni muhimu sanaaa ndani ya Sklight Band anaitwa Daudi Tumba,akizipiga Tumba zake lazima ufurahie

Sam mapenzi (wa kwanza kulia) akiimba kwa upoleeeee kabisaaaa huku akipewa sapoti na Aneth Kushaba(katikati)na Digna Mbepera wa kwanza kushoto.

Yani weweee unanipaaa raahaaa sana ukiwa unaimbaaaa ni shabiki huyu akionyesha mapenzi ya kutoshaaaa kwa Hashimu Donode baada ya kukunwa na uimbaji wake.

Joniko Flower baba ya Congo akiongoza Vijana wake kushambulia jukwaaaa

Sony masamba(katikati) akikamuaaaa sebeneee sebeneeee kwa nguvuu zoteeee

Kama kawaida Skylight Band inavyowapenda mashabiki wake huwa kila Ijumaa shabiki anayesheherekea siku yake ya kuzaliwa hupewa nafasi ya kuimbiwa special Song na kusheherekea na mashabiki wake,Hahahaha si unaona mwenyeweeee hapoooo

Hapo sasa ni viuno, mabega, mikono inahusika kuweza kuyarudi.
20
Nyomiiiii la mashabikiiii wakifurahia muziki mzuriiiii.
21
Kama una furahaaa mikonooo juuuu juuuuuuu.
22
Kikuku huyoooooo.....ana maringooo huyoooo...kwioooo kwiooooo..... Iyo inaitwaga kikukuu ni staili yenye rahaaaaa na utamu unapochezeshwa na Skylight Band.
23
Hiyo staili inaitwaaa sugua suguaaa achaaa ni hatariiiiiiiiii

Mratibu wa Skylight Band Rubeya akishow Love na Mashabiki ndani ya Thai Village

Sam Mapenzi akipata Ukodak na Shabiki wake

Hashimu Donode akipata Ukodak na Mashabiki wake

Skylight band Divas wakifurahia kuapata Ukodak mbele ya kamera yetu
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Posted by Editor on 10:36. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for SKYLIGHT BAND NI MOTO

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery