WAPIGAPICHA MARUFUKU NDANI YA VITUO VYA KURA
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
TUME Huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imepiga marufuku
wapigapicha ndani ya vituo vya kupigia kura, pia haitaruhusiwa kujipiga
picha wakati wakipiga kura.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati, pia amepiga marufuku,
wapigakura kupiga picha karatasi za kupigia kura wakionesha wamemchagua
nani. Ni waandishi wa habari pekee wenye vibali ndio watakaoruhusisiwa
kupiga picha na kuandika habari za uchaguzi ifikapo siku ya uchaguzi
Agosti 8, mwaka huu.
Hata hivyo, waandishi na wapigapicha hao, wataruhusiwa tu kuandika na
kupiga picha mwenendo mzima wa uchaguzi na si vinginevyo. “Upigaji kura
ni kitendo cha siri. Ni makosa kuonesha kila mtu au kutuma kwenye
mitandao ya kijamii umempigia kura nani,” alisema Chebukati.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa katazo hilo limelenga kulinda haki
ya mpiga kura kutunza siri yake kwa mujibu wa Sheria na kuzuia
kushawishi wengine kumpigia kura kiongozi asiyemtaka.
CHANZO HABARI LEO

