MWILI MENEJA TUME YA UCHAGUZI WAPATIKANA
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
Imeandikwa na NAIROBI, Kenya

Mwili wa Meneja huyo ulipatikana ukiwa umehifadhiwa kwenye chumba
kimoja cha kuhifadhi maiti jijini Nairobi. Mawasiliano ya mwisho kutoka
kwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi majira ya saa tisa alfajiri
kupitia ujumbe wa mfupi aliyoyafanya na mmoja wa wafanyakazi wenzake.
Tukio hilo limetokea ikiwa imebaki wiki moja kabla ya kufanyika
uchaguzi mkuu nchini humo, utakaofanyika Agosti 8, mwaka huu. Kwa mujibu
wa Polisi, mwili wa Musando pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa,
ilipatikana eneo la Kikuyu lililopo jijini Nairobi na kupelekwa katika
chumba cha kuhifadhi maiti.
Musando alikuwa akijishughulisha na usambazaji wa vifaa vya
eletroniki ambavyo vingetumiwa kutambua wapiga kura na kutangaza matokeo
wakati wa uchaguzi. Taarifa zinasema kuwa mwili wa Musando ulipelekwa
katika chumba cha kuhifadhi maiti na watu waliojitambulisha kuwa ni
Polisi.
Awali jana, Polisi nchini humo waliliona gari la mkuu huyo wa kitengo
cha Tehama aina ya Land Rover Discovery ikiwa imeegeshwa pembeni ya
barabara inayokwenda kwenye maduka ya Thika na kuivuta hadi katika kituo
cha Polisi cha Kasarani. Kamanda wa Polisi jijini Nairobi, Japhet Koome
alisema tayari gari hilo limechukuliwa kwa ajili ya kukaguliwa alama za
vidole.
Juzi baada ya taarifa kusambaa za kupotea kwa Msando na kutangazwa na
Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati, mmoja wa watumiaji wa ukurasa wa
Twitter aliweka picha za gari la meneja huyo likiwa limeegeshwa
lilipokutwa na Polisi katika eneo la Thika. Familia ya Msando iliripoti
tukio la kupotea kwake katika kituo cha polisi cha Embakasi siku ya
Jumamosi.
CHANZO HABARI LEO
