WAGOMBEA 20 WAJITOKEZA KUWANIA URAIS LIBERIA AKIWEMO MCHEZAJI BORA WA DUNIA
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Rais wa sasa wa Liberia llen Johnson Sirleaf ambaye anamaliza muda wake mwezi October
Wagombea
takribani 20 wanadaiwa kujitokeza katika kuwania kiti cha Urais nchini
Liberia baada ya rais wa sasa Ellen Johnson Sirleaf kutarajiwa kustaafu
baada ya kumaliza muda wake wa miaka 10 ya uongozi.
Kwa
mujibu wa shirika la habari la AFP, limedai miongoni mwa watu watakao
wania nafasi hiyo ni mchezaji bora wa dunia wa zamani George Weah ambaye
pia aliwahi kuwania katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Picha ya George Weah ambaye anatajwa kuwania urais wa Liberia October 10 mwaka huu
AFP
limesema Weah atakuwa akiwania kiti hicho huku makamu wake akiwa ni
Jewel Howard Taylor, 54, ambaye ni mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo
Charles Taylor.
Wagombea
wengine waliotajwa ni Prince Johnson, MacDella Cooper, Makamu wa sasa
wa rais, Joseph Boakai na wengine. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika
October 10 ya mwaka huu.
