WAZIRI MKUU MAJALIWA AITAKA WIZARA YA UTALII KUONGEZA UBUNIFU.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,kushoto akikabidhi Jarida lakutangaza Utalii wa Tanzania Kwa Kiongozi wa maswala ya Utalii katika Mkoa wa Matanzas .Bwana Luis Marines ,jana August 23/2017 wakati alipokuwa katika Ziara ya kikazi kwenye Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nchini Cuba, katikati katika picha ni Mama Mary Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (mwenye miwani)na Mama Mary Majaliwa (kulia) .pamoja na Ujumbe wa Serekali ya Tanzania wakipata maelezo jana August 23/2017kutoka kwa Kiongozi wa Utalii katika Mkoa wa Matanzas ,Bwana Luis Martines. jinsi fukwe za Bahari zinavyo tunzwa nakuwa kivutio kwa Watalii wanao tembelea Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nnchini Cuba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (mwenye shati jeupe) na Mama Mary Majaliwa (kushoto)pamoja na ujumbe wa serekali ya Tanzania jana August23/2017. wakipata maelezo kutoka kwa muongoza wa Talii Bibi Yanseli Marrero kuhusu biashara ya Boti za Utalii kwenye fukwe za Bahari katika Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nnchini Cuba
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kutafuta
mbinu bora za kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini
ili kukuza sekta hiyo.
Amesema
licha ya Tanzania kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini idadi ya
watalii wanaoingia nchini kwa mwaka ni ndogo, hivyo kuna haja ya
kuboresha matangazo.Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Agosti
23, 2017) wakati alipofanya ziara katika mji wa kitalii wa Varadero
ulioko kwenye mkoa wa Matanzas nchini Cuba.
Alisema
mji wa Varadero tu unaingiza watalii zaidi ya milioni moja kwa mwaka na
unategemea kivutio kikubwa kimoja tu cha fukwe ambayo ina urefu wa
kilomita 22.Alisema idadi hiyo ni tofauti na Tanzania ambayo imejaliiwa
kuwa na vivutio vingi vya utalii huku watalii wanaovitembelea ni
wachache. “Tunatakiwa kujitangaza zaidi.”Waziri Mkuu alitaja baadhi ya
vivutio vya utalii ambavyo ni mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, miji
ya kihistoria ya Kilwa, Bagamoyo, Stone Town pamoja na Mikindani.
“Vivutio
vingine ni eneo la Oldvai George ambako binadamu wa kwanza aliwahi
kuishi, hifadhi ya Gombe ambako kuna sokwe ambao wanaishi kama
binadamu.”
Alisema
Serikali itahakikisha jitihada zinafanyika katika kukuza sekta ya
utalii ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vilivyoko nchini ili kuweza
kuongeza idadi ya watalii.Pia Waziri Mkuu aliwahamasisha Watanzania
kujenga tabia ya kutembelea vivutio vyeo vya utalii na kujifunza mambo
mbalimbali na si kuwaachia wageni pekee.Kwa upande wake, Kiongozi wa
Sekta ya Utalii katika mkoa wa Matanzas, Bw. Luis Martinez de Armas
alisema mji wa Varadero ni kivutio kikubwa cha utalii nchini Cuba.
Alisema
kivutio kingine cha utalii ni hoteli zilizojengwa ndani ya bahari,
maeneo ya kihistoria na migahawa inayouza vyakula vya asili vya nchi
hiyo.
Bw.
Luis alisema mwaka 1990 ndio walianza kuendeleza sekta ya utalii katika
mkoa wao na ulikuwa na hoteli 4,436 ambazo kwa sasa zimeongeza na
kufikia hoteli 20,696.
Hata
hivyo Bw. Luis alisema Tanzania inavivutio vingi vya utalii na kwamba
anavutiwa na mlima Kilimanjaro pamoja na wanyama na viumbe vingine
vilivyoko katika mbuga mbalimbali. Alisema wako tayari kushirikiana na
Serikali katika kukuza sekta ya utalii.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 24, 2017.
Posted by Editor
on 12:07.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0