Share this Post

dailyvideo

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AMJULIA HALI MHE. TUNDU LISSU JIJINI NAIROBI



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali leo tarehe 28 Novemba, 2017 jijini Nairobi nchini Kenya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali leo tarehe 28 Novemba, 2017 jijini Nairobi nchini Kenya. Kushoto ni mke wa Mhe. Lissu, Alicia Magabe na kulia ni msaidizi wa Makamu wa Rais Bw. Waziri
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana (kulia) walipofika hospitalini hapo kumjulia hali. Kushoto ni mke wa Mhe. Lissu, Bi. Alicia Magabe na wa pili kulia ni msaidizi wa Makamu wa Rais Bw. Waziri
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali. Kushoto ni mke wa Mhe. Lissu, Bi. Alicia Magabe 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Novemba, 2017 amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake.
Mhe. Tundu Lissu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao.
“Msalimu Mhe. Rais mwambie namshukuru sana kwa salamu zake na kunijulia hali” amesema Mhe. Tundu Lissu.

Posted by Editor on 13:55. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AMJULIA HALI MHE. TUNDU LISSU JIJINI NAIROBI

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery