Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaendelea mjini Bangkok
Washiriki kutoka Tanzania na Kenya wakibadilishana mawazo kuhusu mijadala ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaendelea mjini Bangkok nchini Thailand, (picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais)
======= ======= ======
Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaendelea mjini Bangkok, ambapo leo kundi la 77 na China limekutana kwa mara ya pili na kujadili mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuangalia namna mpango wa kupunguza gasi joto duniani utakavyoweza kufanya kazi.
Katika mkutano wa leo, kundi hilo limejadili pia namna ambavyo nchi zinazoendelea zinapaswa kuainisha taarifa zinazohitajika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabaia nchi, ikiwa ni pamoja na mipango na masuala ya fedha, teknolojia na taaluma.Aidha, washiriki wamejadili kuhusu juhudi za pamoja za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa ujumla na kuwa na hali ya kuweza kufikia malengo ya pamoja ya kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabaia nchi.
Aidha, katika mkutano wa leo umesisitizwa umuhimu wa kila nchi kuwa ‘serious’ katika suala zima la kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua sahihi ili kuweza kufikia malengo ya kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Washiriki pia walitilia mkazo suala la technolojia linavyoweza kuchangia katika athari za mabadiliko ya tabia nchi, na walipata nafasi ya kujadili kwa kifupi kuhusu mkutano wa dunia (COP18) wa mabadiliko ya tabia nchi utakaofanyika mjini Doha mwezi wa Disemba mwaka huu.