NAIBU WAZIRI MKUU ETHIOPIA KUSHIKA MADARAKA HADI UCHAGUZI UTAKAPOFANYIKA.
Mwili wa Wariri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi umelakiwa na maelfu ya watu waliokuwa wakilia wakati wa kipindi rasmi cha maombolezo kikianza baada ya kifo cha kiongozi huyo katika hospitali mjini Brussels.
Bendi ya jeshi ilipiga nyimbo za maombolezo wakati jeneza , lililofunikwa bendera ya taifa , likitolewa kutoka katika ndege ya shirika la ndege la Ethiopia tukio ambalo pia lilihudhuriwa na viongozi wa kisiasa , kidini na jeshi pamoja na wanadiplomasia.
Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn, mwenye umri wa miaka 47, ambaye pia ni waziri wa Mambo ya Nje tangu mwaka 2010, ataongoza nchi hiyo kwa muda.
Vyombo vya habari vya taifa vimeripoti kuwa kiongozi huyo atabakia madarakani hadi uchaguzi wa mwaka 2015, licha ya kuwa huenda baadaye mwaka huu.
Meles Zenewi amefariki usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne kufuatia kuugua kwa muda mrefu.