Share this Post

dailyvideo

MAAFA: ALGERIA YAANZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO, BAADA YA WATU WENGI KUFARIKI KATIKA AJAL YA NDEGE.I.





Ndege iliyoanguka Algeria

Algeria imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia kuuawa kwa watu sabini na saba kwenye ajali iliyohusiha ndege moja ya Kijeshi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Abiria mmoja alinusurika ajali hiyo iliyohusisha ndege aina ya Hercules C-130 iliyoanguka katika eneo la milima ya Oum al-Bouaghi, ikiwa njiani kuelekea mji wa Constantine.


Ripoti zinasema hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hiyo ya ndege.

Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika amewasifu wanajeshi waliopoteza maisha yao na kuwataja kama wafia dini wa taifa hilo.

Wengi wa abiria sabini na nane waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni maafisa wa kijeshi na familia zao.


Mabaki ya ndege ya jeshi la Algeria iliyoanguka


Mwanajeshi aliyenusurika, anaripotiwa kuendelea kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Constantine kufuatia majeraha ya kichwa.

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa imeunda tume maalum kuchunguza ajali hiyo na kuwa Ahmed Gaid Salah, ambaye ni mkuu wa majeshi nba naibu waziri wa Ulinzi atazuru eneo la ajali hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, wizara ya ulinzi imesema kuwa hali mbaya ya anga iliyohusisha kimbunga na mvua kubwa ya barafu ilisababisha ajali hiyo.

Runinga ya taifa ilionyesha picha za ajali hiyo.


Awali maafisa wa Ulinzi na shirika hilo la habari liliripoti kuwa watu 103 walikuwa ndani ya ndege hiyo lakini idadi hiyo ilipunguzwa hadi watu sabini na nane.Chanzo BBC Swahili



Posted by Editor on 12:16. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for MAAFA: ALGERIA YAANZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO, BAADA YA WATU WENGI KUFARIKI KATIKA AJAL YA NDEGE.I.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery