. KUPITISHWA KWA SHERIA YA KUHARAMISHA USHOGA, UGANDA YANYIMWA DOLA 90 NA BENKI YA DUNIA ILIYOKUWA IMARISHE SEKTA YA AFYA.
RAIS YOWERI MUSEVEN.
BENKI
ya dunia imesitisha mkopo wa dola milioni 90 kwa Uganda wa kuimarisha
sekta ya afya kufuatia kupitishwa kwa sheria inayoharamisha ushoga na
kutoa adhabu kali kwa watakaopatikana na hatia.
Hatua hiyo ya benki
ya dunia haikutarajiwa na wengi kwani taasisi hiyo mara nyingi
hujiepusha kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa ya nchi wanachama au
kuhusiana na masuala kama haki za mashoga, kuepuka kuzishurutisha nchi
wanachame wake 188.
Hata hivyo msemaji wa benki hiyo
David Theis amesema katika barua pepe kuwa wamesitisha mradi huo wa
kuboresha sekta ya afya ya Uganda hadi watakapoufanyia tathmini na
kuhakikisha malengo yake ya maendeleo hayataathiriwa na sheria hiyo mpya
ya kuharamisha ushoga.
Rais wa benki hiyo Jim Yong Kim
amewatumia wafanyakazi wake barua akisema benki ya dunia inapinga
ubaguzi na itawalinda wafanyakazi wake wote na kuongeza kupitishwa kwa
sheria hiyo ya Uganda sio nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani ushoga
umeharamishwa katika nchi 83 na zaidi ya nyingine 100 zinawabagua
wanawake.
Mkopo ulikuwa uimarishe sekta ya afya
Licha ya kusimamishwa kwa mkopo huo wa dola milioni 90,benki ya dunia
bado ina miradi mingine nchini Uganda ya kiasi cha dola bilioni 1.56.
Mkopo huo ulitarajiwa kuidhinishwa hapo jana na ulipaswa kuangazia
miradi ya kuboresha afya ya uzazi,afya ya watoto wachanga na uzazi wa
mpango.
Kutiwa saini kwa sheria hiyo ya
kuharamisha ushoga Uganda na Rais Yoweri Museveni mapema wiki hii
kumeibua shutuma kali kutoka kwa nchi za magharibi na mashirika ya
kutetea haki za binadamu.
Norway,Denmark na Uholanzi
zimetangaza kuwa zitasitisha misaada kwa serikali ya Uganda kutokana na
sheria hiyo na nchi nyingine wafadhili ikiwemo Marekani pia zimetishia
kusitisha misaada na kutafakari upya uhusiano kati yao na Uganda.
Ghadhabu hiyo ya nchi za magharibi
kuhusu kuharamishwa kwa ushoga ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha
gerezani kwa watakaokutikana na hatia imeporomosha thamani ya shilingi
ya Uganda na kusababisha Benki nchini humo kuingilia kati kwa siku mbili
mfululizo.
Kutiwa saini kwa sheria hiyo ya
kuharamisha ushoga Uganda na Rais Yoweri Museveni mapema wiki hii
kumeibua shutuma kali kutoka kwa nchi za magharibi na mashirika ya
kutetea haki za binadamu.
Norway,Denmark na Uholanzi
zimetangaza kuwa zitasitisha misaada kwa serikali ya Uganda kutokana na
sheria hiyo na nchi nyingine wafadhili ikiwemo Marekani pia zimetishia
kusitisha misaada na kutafakari upya uhusiano kati yao na Uganda.
Ghadhabu hiyo ya nchi za magharibi
kuhusu kuharamishwa kwa ushoga ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha
gerezani kwa watakaokutikana na hatia imeporomosha thamani ya shilingi
ya Uganda na kusababisha Benki nchini humo kuingilia kati kwa siku mbili
mfululizo.
Serikali ya Uganda haina wasiwasi
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amesema Uganda
inaweza kujiendeleza bila ya misaada kutoka nchi za magharibi na
kuongeza Uganda haina wasiwasi na hatua hizo kwani ni wakati kwa Afrika
kupinga ukoloni, utumwa na ubabe kutoka magharibi.
Mwanaharakati ambaye amekuwa katika
mstari wa mbele kuwatetea mashoga nchini Uganda Frank Mugisha alikutana
na maafisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini
Washington hapo jana kuomba usaidizi utakaowalinda mashoga.
Ofisi ya kutetea haki za binadamu
ya Umoja wa Mataifa umelaani kuchapishwa kwa majina ya watu wanaodaiwa
kuwa mashoga nchini Uganda katika gazeti moja la udaku nchini humo na
kuonya hatua hiyo inakiuka haki ya kuwa na faragha na kuonyesha wazi
kuwa maisha ya mashoga yamo hatarini.
Kiongozi wa upinzani Uganda Kizza
Besigye ameishutumu serikali kwa kutumia suala hilo kuwahadaa raia wa
nchi hiyo ili wasiangalie masuala muhimu kama ufisadi au kuwepo kwa
jeshi la Uganda Sudan Kusini.(E.L)