NORWAY YAIFUTIA UGANDA MSAADA
Sheria
hiyo iliwaudhi viongozi wa nchi za Magharibi, ikiwamo Marekani, ambayo
Rais wake, Barack Obama alieleza kuwa inafaa kuangaliwa upya.
Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa mpinzani mkubwa wa vitendo vya ushoga, alisaini sheria hiyo Jumatatu wiki hii.
“Sheria
hii mpya inapinga haki za msingi za binadamu na pia inakiuka katiba ya
nchi hiyo (Uganda),’’ alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Borge
Brende.
Aliongeza:
“Tutazuia msaada wa Kroner 50 milioni (Sh 20 bilioni za Uganda) na
tutaongeza jitihada zetu na nguvu zote na ushirikiano katika masuala ya
haki za binadamu na kuhakikisha demokrasia inalindwa nchini Uganda.
Waziri huyo alitoa tamko hilo kupitia kwa msaidizi wa Balozi wa Norway nchini Uganda, Kyree Holm
“Rais
(Museveni) alisaini muswada huo ambao unatoa adhabu kali kwa mtu yeyote
atakayekutwa na hatia ya kufanya vitendo vya uhusiano wa jinsia moja,
sheria ambayo inakiuka misingi ya raia wa nchi yake,” alisema Holm.
Naye
Mkurugenzi wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya (EU), Catherine Ashton
alisema kwamba kilichofanyika Uganda ni ubabe kwani huwezi kutoa kifungo
cha maisha kwa kuwa na uhusiano wa jinsia moja.
Muswada
wa kupiga marufuku uhusiano wa watu wa jinsia moja ulipitishwa Desemba
mwaka jana na Bunge la Uganda baada ya mjadala mkali.
Miongoni
mwa vipengele vya muswada huo, ni vile vinavyotoa amri ya kufungwa jela
maisha kwa mtu atakayekutwa na hatia ya kuwa na uhusiano huo, ikiwa ni
pamoja na wale wanaohamasisha na vitendo hivyo.
Rais Obama
alitishia kuwa uhusiano wa Uganda na nchi yake utaharibika kutokana na
hatua ya Rais Museveni kusaini muswada huo na kuufanya kuwa sheria.
Muungano wa vyama vya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda umeazimia
kuandaa sala ya pamoja ambayo wameiita ya amani ya kuiombea dua
Serikali ya nchi yao baada ya kupitisha muswada huo kuwa sheria
Posted by Editor
on 09:32.
Filed under
eastafricannews
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0